Ruka hadi kwa yaliyomo kuu
Uhamaji

Ukarabati na matengenezo

Somo: la 4 kati ya masomo 5
Mada: 3 kati ya Mada 4
0% Imekamilika

kama kifaa saidizi kimekarabatiwa au kubadilishwa, Kumbuka kwamba kinapaswa kurekebishwa na na kupata kipimo shaihi cha mhusika.

viatu tibavyenye sehemu iliyoharibika

viatu tiba vyenye sehemu iliyoharibika vinapaswa kukaguliwa na mtoa huduma.

Mjulishe mhusika kuwa anaweza kuwasiliana nawe kama kiatu tiba kitaharibika.

Aina za uharibifu zilizozoeleka

Uharibifu wa kawaida uliozoeleka unaoweza kurekebishwa ni:

  • Kapeti la ndani ya kiatu iliyoharibika
  • Sehemu ambazo kamba inashika hazifai tena
  • Kuchanika kwa kamba
  • Kuchanika kwa sehemu ya juu ya kiatu
  • Soli iliyharibika

namna ya kukarabati kiatu tiba kilichoharibika

Ni lazima ukarabati wa kiatu tiba ufanywe na mtaalamu aliyepata mafunzo.  Haupaswi kuhitajika Kurekebisha viatu tiba.

Utaratibu wa ukarabati utategemea huduma za ukarabati zinazopatikana sehemu kiatu saidizi kinapotumika.

Shughuli za ukarabati ambao ni rahisi, kama vile kubadilisha kamba yenye urefu unaoweza kuongezwa au kupunguzwa, inaweza kufungwa na mtengenezaji wa viatu wa eneo ambapo kiatu kinatumika au kwenye huduma ya kukarabati viatu.

Kubadilisha viatu tiba

Badilisha na upate kipimo sahihi cha viatu tiba kwa mara nyingine kama:

  • Hakimtoshi tena mvaaji
  • viatu vimeharibika na haviwezi kukarabatiwa.

 Swali

Jospehina amenyanyua mguu wake ili Mhudumu wa afya aweze kuangalia viatu tiba.

UnamKumbuka Josephina?

Josephina amekuwa akivaa viatu tiba vyake ambavyo viko wazi kwa muda wa miezi 12. Sasa inaonekana kuna sehemu ya viatu imeharibika.

Kamba za viatu ambazo zinazoweza kurekebishwa zimechanika na hazifai tena kufunga viatu.

Josephina anapaswa kufanya nini?



Umepatia iwapo umechagua majibu sahihi kuwa ni "a" na "b"

Ni bora Kurekebisha sehemu za kiatu ambazo zinaweza kurekebishika, Hakikisha kuwa unapata kipimo sahihi, ulinzi pamoja na Msaada wa kutosha.

c Sio sahihi.

Ikiwa hivi ndio viatu tiba pekee alivyonavyo Josephina, anapaswa kuviRekebisha haraka iwezekanavyo lakini, lakini aendelee kuvivaa.

Josephina hapaswi kuvaa viatu vilivyoharibika Ikiwa ana viatu vingine vya kuvaa. Kamba za viatu  zina kazi muhimu katika uvaaji wa viatu. Kamba iliyoharibika inaweza kumfanya asifunge viatu vizuri na kusababisha uwepo wa kidonda cha mguu.