Katika mada hii utaongeza ujuzi juu ya kile ambacho tayari umejifunza kuhusu majeraha kwenye miguu na viatu vinavyofaa kuvaliwa.
Ikiwa hukumbuki dalili mbaya za jeraha la mguu, au hauna uhakika, rudia kupitia Mada zilizotangulia za majeraha ya miguu katika Moduli ya vifaa saidizi vya kusogea kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine.
Ikiwa hukumbuki sifa vya viatu vinavyofaa, au huna uhakika, rudi nyuma na upitie Mada ya kufundisha katika Moduli ya vifaa saidizi vya kusogea kutoka eneo moja kwenda eneo lingine vya TAP.
viatu tiba ni nini?
Duniani kote Kila baada ya Sekunde thelathini mtu anakatwa Linki kutokana na ugonjwa wa kisukari. Sababu nyingi za kukatwa viungo hivi hutokea baada ya jeraha la mguuni kuwa katika hali mbaya.
viatu tiba ni viatu vyenye vitu maalum vinavyosaidia kulinda na kusaidia miguu ya mhusikamiaji. Hupunguza hatari ya mhusikamiaji kupata jeraha la mguuni.

Nani anaweza kufaidika na viatu tiba?
Watu walio katika hatari kiasi ya kupata majeraha kwenye miguu ambao hawana jeraha la miguu Wanaweza kufaidika na matumizi ya viatu tiba.

Kutana na Jensen
Jensen ana umri wa miaka 60 na ana ugonjwa wa kisukari.
ugonjwa wa kisukari wa Jensen unamweka katika hatari ya kupata jeraha la mguu. Mhudumu wa afya alimfanyia kipimo cha miguu na kugundua kuwa Jensen yuko katika hatari kubwa.
Mhudumu huyo wa afya alibaini kuwa Jensen ana hatari kubwa ya kupata jeraha la mguu.
Jensen anaweza kufaidika na viatu vya tiba kwa:
- Kulinda na kusaidia miguu yake Wakati wa kutembea
- Kuzuia jeraha la mguu.
viatu vinavyofaa
Watu walio katika hatari ndogo ya kupata majeraha kwenye miguu wanASHAuriwa kuvaa viatu vinavyofaa.

Swali
Sifa za viatu vinavyofaa zimeelezewa katika Moduli ya vifaa saidizi vya kuhama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine. Pima Uwezo wako wa KuKumbuka sifa hizo hapa chini.
Ni sifa zipi kati ya hizi zifuatazo kiatu kinachofaa kinapaswa kuwa nazo?
Chagua majibu sahihi tu.
Umepatia iwapo ulionyesha kuwa majibu yote yako sahihi. Kila sifa iliyopo inapaswa kuwepo kwenye kiatu kinachofaa.
Ikiwa haukuchagua sifa zote, au haukuwa na uhakika, rudia Kusoma Moduli ya vifaa saidizi vya kuhama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine vya TAP na ili uweze kurejesha kumbukumbu yako vizuri.
Watu ambao tayari wana jeraha mguuni
viatu tiba havitumiwi kutibu au kusimamia jeraha la sasa la mguu.
majeraha kwenye miguu Yanahitaji usimamizi wa kitabibu na kusafishwa mara kwa mara. Aidha mtu mwenye kidonda, anaweza kuweka kitu ndani ya kiatu ili kupunguza msuguano wa kiatu na kidonda.
Watu wenye jeraha kwenye mguu wanapaswa kupelekwa kliniki ya jeraha la mguu.
