Ruka hadi kwa yaliyomo kuu
Uhamaji

ufuatiliaji wa kiatu kigumu saidzi

Somo: la 4 kati ya masomo 5
Mada: 1 kati ya Mada 2
0% Imekamilika

Mara nyingi viatu vigumu saidizi  vinatumika kwa Muda mfupi. Sio kila mtu atahitaji kufuatiliwa na Mhudumu wa afya.

Watu wengi watafuatiliwa na daktari wao aliyewapa rufaa Ikiwa wana:

  • Uwezo wa kuhama vizuri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
  • Uwezo mzuri wa kuhisi
  • Hawana matatizo ya ngozi.

Ikiwa mtumiaji ana tatizo lolote, anapaswa kufuatiliwa ndani ya Wiki moja.

Wei ameketi chini wakati mtoa huduma wa afya akipima ukubwa wa kiatu chake kigumu  kulingana na mguu wake

Soma zaidi ili uJifunze zaidi kuhusu lini watumiaji wa viatu saidizi watafaidika kabla ya kurudi kwa daktari aliyewapa rufaa.

Swali

Mario Wakati wa amevaa kiatu kigumu saidizi huku akifanya mahojiano na Mhudumu wa afya wakati alipofanyiwa ufuatiliaji.
UnamKumbuka Mario?

Mario alikuwa akitumia kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa baada ya upasuaji wa kifundo cha mguu. Mario ana ugonjwa wa kisukari na Matatizo ya hisia katika miguu yake.

Hivi karibuni Mario amepewa kiatu kigumu kinachomkaa vizuri.

Je ni lini anapaswa kufanyiwa ufuatiliwaji?




uko sahihi iwapo umechagua jibu kuwa ni "a".

Mario anapoteza hisia (hisia\) miguuni mwake, hivyo yuko katika hatari ya kupata majeraha kwenye miguu. Anapaswa kufuatiliwa Wiki moja baada ya kuanza kutumia kiatu kigumu saidizi ili kuhakikisha kuwa hakimsababishi Matatizo yoyote.

Umekosea kama umechagua "b, c au d".

Kufanyauufuatiliaji baada ya muda wa wiki Nne au sita, ni Muda mrefu sana. Mario anapaswa kufuatiliwa mapema kwa sababu yuko katika hatari ya kupata Matatizo ya miguu.

Daktari pia atafanya ufuatiliaji pale ambapo Mario hahitaji kiatu kigumu saidizi.

UFuatilia baada ya Wiki moja

Kagua:

  • Kiatu kigumu saidizi hakisababishi shida yoyote kwa watu wenye Matatizo ya ngozi au Matatizo ya hisia (hisia\) miguuni mwao.
  • Kiatu kigumu saidizi kinawakaa vyema, watu wenye uvimbe.
  • mtumiaji wa kaitu kigumu anaweza kutembea vizuri na kiatu kigumu saidizi kama utakuwa unahofia Uwezo wake wa kutembea bila kutetereka.

Swali

Mario Wakati wa amevaa kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa akihojiwa na mtoa huduma ya afya Wakati wa mahojiano ya ufuatiliaji

UnamKumbuka Mario?

Wakati wa ufuatiliaji wa kwanza wa Mario, alisema kuwa anakaa nyumbani kwa sababu anapata taabu kutumia viatu vigumu vinavyoweza kuvuliwa nje ya nyumba.

Waweza kumsaidiaje Mario?

Chagua majibu sahihi tu.



Umepatia iwapo umechagua majibu sahihi kuwa ni "a" na "b"

KuMwangalia Mario akitembea nje ya jengo; kutakusaidia kuamua kama anahitaji kifaa saidizi cha kutembelea ili aweza kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine au hahitaji.

Mario akitembea na fimbo ya kutembelea huku Wakati wa amevaa kiatu kigumu.

Wakati alipofanyiwa ufuatiliaji kwa mara ya kwanza, Mario hakuonekana au kujisikia kama anaweza kutembea nje bila kuanguka.mtoa huduma ya afya wa Mario aliamua kumfanyia tathmini ili kujua kama anaweza kupata kifaa kinachoweza kumsaidia kutembea.

Sasa anatumia fimbo ya kutembelea ili aweze kufanya hivyo. Pia anajiamini zaidi wakati anapotumia kiatu kigumu nje ya nyumba yake na anaweza kwenda duka lililo karibu na anapoishi

Swali

Wei ameketi chini wakati mtoa huduma wa afya akipima ukubwa wa kiatu chake kigumu  kulingana na mguu wake

UnamKumbuka Wei?

Wei aliita na kuomba kufanyiwa ufuatiliaji kwasababu kiati chake kigumu kilianza kupwaya. Alipoteza kamba mojawapo ya kiatu.

Utafanya nini kumsaidia Wei?

Chagua majibu sahihi tu.



Umepatia iwapo umechagua majibu sahihi kuwa ni "a" na "b"

Badilisha kamba za viatu zilizopotea. kama kiatu kigumu saidizi hakimtoshi vizuri mvaaji baada ya kubadilisha kamba za viatu, badili kiatu hiki na utumie kiatu kipya.

c Sio sahihi.

Unahitaji kuangalia vizuri kabla ya kubadilisha kiatu chenye ukubwa tofauti.

ufuatiliaji baada ya wiki sita

mtu anayetumia kiatu kigumu saidizi kwa Muda mrefu zaidi ya wiki sita anapaswa kufuatiliwa na baada ya wiki sita.

Wakati wa ufuatiliaji huu, angalia kama kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa kimechakaa au kimekatika

Kagua:

  • Kamba za kufungia kiatu zipo na hazijakatika
  • Soli iko katika hali nzuri.

Baada ya wiki sita, sehemu ya ndani ya kiatu itakuwa chafu. Unaweza kuibadilisha utakapoenda kufanya ufuatiliaji.

Kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa chenye kamba za kukifunga vizuri ambazo zina Majina kIkiwa katika hali nzuri, sehemu ya chini haijachakaa na sehemu ya ndani ya kiatu iko katika hali nzuri

Utahitaji kubadilisha kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa kama kimekatika, au kama soli yake imekatika

Ikiwa kifaa kimerekebishwa au kubadilishwa, lazima mhusika avalishwe tena kupata kipimo sahihi kwake