Ruka hadi kwa yaliyomo kuu
Maono

Matatizo ya kuona ambayo hayawezi kuboreshwa

Somo: la 1 kati ya masomo 4
Mada: 4 kati ya Mada 4
0% Imekamilika

Baadhi ya matatizo ya kuona hayawezi kuboreshwa. Hii ina maana kwamba kuona hakuwezi kurejeshwa kikamilifu kwa matibabu au miwani ya dawa.

Watu wengi walio katika hali hii waweza kuwa na uoni hafifu au upofu. vifaa saidizi ni muhimu sana kwa kundi hili la watu.

uoni hafifu

mtu mwenye uoni hafifu anaweza kuona baadhi ya vitu lakini kwa kawaida hupata shida kujifunza au kutekeleza majukumu bila kuwa na vifaa sadizi vya uoni kwa watu wenye uoni hafifu.

Sababu tofauti za uoni hafifu zInaweza kusababisha Matatizo katika kufanya kazi tofauti. Kwa mfano:

  • Watu wenye tatizo kuu la Kupoteza uwezo wa kuona vitu vilivyo moja kwa moja Wakati wa yao) waTAPata shida kuona vitu au watu kwa kina.
  • Watu waliopoteza Uwezo wa kuona pembeni (Kupoteza uwezo wa kuona vitu ambavyo viko pembezoni mwa uoni wao) wanaweza kupata taabu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, kwani kuona ardhi iliyoko sehemu ya chini waliopo na vikwazo vyovyote ni vigumu.

Watu wenye tatizo la kuona vibaya wanapaswa kufanyiwa tathmini kamili ya uwezo wao wa kuona na mtaalamu wa afya ya macho; kwani miwani ya dawa na huduma nyingine za kimatibabu zinaweza kuboresha uwezo wao wa kuona.

Ying anatumia kifaa cha kukuza sauti kinachoshikiliwa kwa mkono pamoja na miwani yake ya dawa kusoma kipande cha karatasi.

Kutana na Ying

Ying anafanya kazi ofisini. Anavaa miwani ya dawa. Hii huboresha uwezo wake wa kuona, lakini bado hawezi kuona kwa mbali.

Mbali na miwani yake ya dawa, Ying anatumia kikuzaji cha mkono kuona vitu kwa karibu na darubini kuona vitu vilivyo mbali zaidi.

Ying akiwa amevaa miwani yake ya dawa anatumia darubini.

Swali

Unadhani Ying ana shida gani ya kuona?

  • Tatizo la kuona mbali (myopia)
  • Tatizo la kuona karibu (hyperopia)
  • Astigmatism
  • Tatizo la kuona karibu kwa wazee (presbyopia)
  • uoni hafifu

Ying ana uwezo mdogo wa kuona kwa sababu tatizo lake la kuona haliwezi kurekebishwa kikamilifu kwa kutumia miwani ya dawa.

Upofu

mtu ambaye ni kipofu anapoteza Uwezo mkubwa wa kuona.

mtu yeyote ambaye ni kipofu anapaswa kufanyiwa tathmini kamili ya uoni wake na mtaalamu wa afya ya macho. Upofu wao Unaweza kusababishwa na tatizo la kiafya la macho ambalo linaweza kutibiwa ili kuboresha au kurejesha uoni wao.

Watu ambao ni vipofu kabisa hutumia njia tofauti kujifunza na kufanya shughuli zao, mara nyingi hufanya shughuli zao kwa kutumia vifaa saidizi.

Watoto na Watu wazima wenye Matatizo yoyote ya uoni waliyoelezwa hapo juu Wanaweza kufaidika na vifaa saidizi vya uoni.

Kifaa kipi au vifaa vipi vinategemea tatizo la uoni walilio nalo na vitu wanavyotaka kufanya.

Umekamilisha somo la kwanza!