Kabla ya kuanza upimaji

Maendeleo ya usoMaji Mada:

Programu ya upimaji kwa watoto wenye umri wa kwenda shule inahusisha kupanga vizuri kila hatua.

Maelekezo

Katika mada hii utajifunza kuhusu hatua zinazohusika katika kuanzisha programu ya upimaji.

Kuandaa programu ya upimaji

Kabla ya kutekeleza mpango wa upimaji, ni muhimu:

  • Kupata idhini kutoka kwa Wizara ya Afya (MoH) na Wizara ya Elimu (MoE)
  • Kuainisha maeneo yenye uwezo wa kufanya programu ya upimaji, ikiwemo wafanyakazi na mazingira yanayofaa
  • Kutambua njia na michakato ya rufaa kwa huduma za za macho na masikio zinazopatikana eneo husika
  • Kuanisha wapimaji na kuwapa mafunzo
  • Vifaa vya kufanya upimaji.

Swali

Kwa nini ni muhimu kuwa na uhusiano na wahudumu wa huduma ya macho na masikio walio karibu na eneo analoishi mgonjwa; wahdumu ambao ndio watapokea rufaa zako?

Chagua majibu sahihi tu.




Ikiwa umechagua a, b na c uko sahihi!

Kupitia mchakato wa upimaji utatambua watoto wanaohitaji rufaa kwa wafanyakazi wa huduma ya macho baada ya siku ya upimaji.

d Sio sahihi.

Wafanyakazi wa karibu wa huduma ya macho na masikio wanaweza kupatikana ili kuwashauri wachunguzi wakiwa mbali au ana kwa ana siku ya upimaji. Hawatafanya upimaji.

Kuratibu upimaji

Ili kuratibu upimaji mkuu wa shule (au mtu mwingine mwenye aliyepewa wajibu huo) na mpimaji wanapaswa kuKutana na:

  • Kuainisha wafanyakazi wengine ili kusaidia katika upimaji ikiwa ni pamoja na:
    • Mratibu wa upimaji shuleni
    • Wasaidizi wa upimaji
  • Kuainisha na kuandaa nafasi ya upimaji
  • Kuandaa nyaraka
  • Kuwapanga watoto.

Kutana na Ayana na Jabari

Ayana anafanya kazi katika shirika la eneo analoishi kama mpimaji wa hisia za uoni na kusikia. Ayana anaKutana na mkuu wa shule wakati akishiriki katika programu ya upimaji wa hisia za uoni na uwezo wa kusikia eneo hilo.

Mkuu wa shule anamteua Jabari kuwa mratibu wa upimaji.

Kwa pamoja, Ayana na Jabari:

  • Wanapata ruhusa ya kutumia vyumba viwili siku ya upimaji ikiwa ni pamoja na ukumbi mkuu na darasa
  • Wanachapisha fomu na orodha ya vitu vya upimaji
  • Wanaanisha walimu na wazazi ili kusaidia kwenye siku ya upimaji
  • Wanajadili jinsi ya kuandaa na kupanga watoto kwa ajili ya upimaji.

Swali

Je, unafikiri ni mambo gani ya kuzingatia wakati wa kuchagua sehemu ya kufanyia upimaji wa uoni na kusikia?

1. Kiwango cha kelele zinazotoka nje

Sahihi!

Kelele za kutoka nje zinafanya iwe vigumu kwa mtoto kusikia sauti za wakati wa upimaji wa kusikia. Ni muhimu kutafuta nafasi ambayo haina kelele za nje ili ili kupata matokeo sahihi.

2. Chumba chenye mwanga wa kutosha

Sahihi!

Ili kuweza kuona vizuri chati za uoni , ni muhimu kuwa na chumba chenye mwanga wa kutosha.

3. Ukubwa wa chumba

Sahihi!

Ili kufanya upimaji wa uoni lazima kuwe na nafasi ya kuweka kiti walau kwa umbali wa mita 3 kutoka kwenye chati ya uoni.

4. Vifaa vya kunawia mikono

Sahihi!

Ni muhimu kwa mpimaji kunawa mikono kabla na baada ya kupima macho au kuangalia afya ya masikio ili kuepuka hatari ya kupata maambukizi.

5. Nafasi kwa ajili ya watoto wote

Sio sahihi.

Ili kupata matokeo sahihi watoto watapimwa mmoja baada ya mwingine. Mtoto mmoja tu atakuwa chumbani kwa wakati mmoja.

Mambo ya kuzingatia kwenye kujumuisha wengi

Watoto wote wanapaswa kuwa na uwezo wa kufanyiwa upimaji. Hii ni pamoja na watoto walio na matatizo ya kuona na kusikia ambayo tayari yanayojulikana na wale walio na mahitaji ya kimwili na mahitaji ya kujifunza.

Jadili na mratibu wa upimaji wa shule jinsi ya kuwezesha upimaji kwa watoto wote wenye mahitaji ya ziada na uweke mpango mzuri ili kukamilisha hili.

Fikiria eneo la nafasi ya upimaji na haja ya mtu mzima mzima kuongozana na mtoto.

Kutana na Aleisha

Aleisha standing with her posterior walker, a four-wheeled frame supporting her from behind for her to hold onto at her sides. She is also wearing ankle foot orthosis which are supportive braces on her ankles.

Aleisha hawezi kupanda ngazi. Shule yake ilipanga Upimaji wa hisia za kusikia na kuona ufanyike nyumba ya chini ya jengo la ghorofa ili aweze kushiriki.

Kutana na Eka

Eka ana matatizo ya kujifunza. Hakuweza kushiriki katika upimaji wa hisia za uoni na uwezo wa kusikia uliofanyika shuleni kwa sababu anapata ugumu kuelewa na kufuata maelekezo. Alipewa rufaa kwenda kuonana na mtaalam wa huduma ya macho na masikio ambaye ana uzoefu wa kuwapima watoto walio na aina hii ya matatizo.

Idhini

Kabla ya kufanya Upimaji wa hisia za kusikia na kuona, ni muhimu kupata idhini kwa kila mtoto kutoka kwa mtu aliyeidhinishwa. Huyu anaweza kuwa wazazi/walezi au mkuu wa shule.

Kuomba ridhaa kutoka kwa wazazi/walezi, shule inaweza kutumia fomu ya ridhaa.

Hii ni pamoja na:

  • Taarifa za msingi kuhusu programu ya upimaji na yale yaliyomo
  • Maswali rahisi kwa wazazi/walezi ambayo hutoa taarifa muhimu kwa ajili ya upimaji.

Mwongozo wa eneo husika unapaswa kufuatwa wakati wa kutafuta idhini kutoka kwa familia ambazo haziwezi kusoma au kuweka sahihi kwa maandishi.

Maelekezo

Ikiwa bado hujafanya hivyo, chapisha fomu ya ridhaa . Unaweza pia kupata fomu hiyo katika kitabu cha utekelezaji wa upimaji wa uoni na kusikia kwa watoto wenye umri wa kwenda shule .

Mara tu idhini inapopokelewa inabainishwa katika mfumo wa kumbukumbu za shule kuhusu upimaji wa hisia za kusikia na kuona.

Ikiwa ridhaa haijatolewa, mratibu wa upimaji shuleni anapaswa kuzungumza na wazazi/walezi ili kujaribu na kujua sababu za kutokubali kwao

Wazazi wanaweza kuhitaji taarifa zaidi kuhusu upimaji na kupewa uhakika kuwa upimaji hautakuwa ma madhara yoyote kwa mtoto.

Dokezo

Wazazi/walezi wanapaswa kuruhusiwa kuhudhuria upimaji wa mtoto wao, kama itawezekana.

Unapojitayarisha kwa upimaji, kagua kama kuna mapngo au programu zozote zinazopatikana karibu na eneo unaloishi; ambazo zinatoa huduma kwa bei nafuu zaidi au pengine bila malipo yoyote kwa watoto wowote wanaohitaji rufaa.

Majadiliano

Wazazi/walezi wanaweza kuwa na dukuduku gani kuhusu mtoto wao kushiriki katika upimaji wa hisia za kuona na kusikia?

  • Hofu ya mitazamo hasi kutoka kwa wengine ikiwa shida haitaweza kujulikana
  • Hofu ya gharama za kupata huduma ikiwa mtoto wao atapewa rufaa
  • Dukuduku kuhusu kama wataweza kuruhusiwa kutokwenda kazini ili kumpeleka mtoto wao kwenye huduma ikiwa mtoto atakua amepewa rufaa.

Namna gani unaweza kuwahakikishia wazazi na kuwatia moyo kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika upimaji?

  • Wahakikishie kuwa unaelewa wasiwasi wako kuhusu namna ambavyo wengine wanavyoweza kuchukulia jambo hili, lakini matatizo ya kuona na kusikia ni ya kawaida sana, na kupata msaada si jambo la kuonea aibu.
  • Eleza kwamba kutambuamapema matatizo ya kuona na kusikia ni njia bora mojawapo ya kusaidia mtoto kujifunza, kujiamini na ustawi wake kwa ujumla.
  • Washauri wazazi ikiwa kuna huduma katika eneo lao zinazopatikana kwa bei nafuu zaidi
  • Hakiki kama kuna uwezekano huduma zikapatikana miadi ya jioni au miadi ya wikendi.