Pakua fomu ya rufaa kwenda kupata viatu vigumu saidizi na uvidole vya mguuni nakala; kama bado hujafanya hivyo
Uiswe na wasiwasi iwapo huwezi kupakua fomu. Sehemu muhimu za fomu zimeonyeshwa na kuelezewa vizuri hapa chini.

Fomu ya rufaa iliyotambulishwa kwenye Mada hii hutoa mfano wa taarifa muhimu zaidi unazopaswa kuwa nazo Wakati wa kutoa rufaa.
Swali
Je, kauli hii ni ya kweli au sio ya kweli?
Ni salama kumpa mhitaji kiatu kigumu saidizi bila ya kupata rufaa kutoka kwa daktari.
Umekosea, iwapo umechagua Sio kweli kama ndio Jibu sahihi
Sio salama kugawa kiatu kigumu saidizi bila ya kupata rufaa kutoka kwa daktari.
Daktari atatathmini kama Hii ni bidhaa sahihi kwa mhitaji.
kama kiatu kigumu saizi hakifai kwa mhitaji, hakitamsaidia kupona jeraha lake na inaweza kufanya hali yake kuwa mbaya zaidi.
Swali
Ni kwa uharaka gani mhitaji wa kiatu kigumu saidizi anapaswa kupewa kiatu hicho baada ya kupata rufaa?
Sahihi.
mtu anapaswa kupewa kiatu kigumu saidizi mara moja ili kumsaidia kupona jeraha lake.
Sio sahihi.
Mhitaji hawezi kusubiri kwa Wiki moja. Bila kupata Msaada na ulinzi, jeraha lake linaweza kuwa na hAli mbaya zaidi.
Sio sahihi.
mtu hawezi kusubiri kwa Mwezi mmoja. Ucheleweshaji kwa Mwezi mmoja Unaweza kusababisha hAli ya majeraha kuwa mbaya zaidi.
Majadiliano
Je, unapokea rufaa nyingine yoyote katika kazi yako ambapo mhitaji anapaswa kupewa huduma Siku hiyo hiyo?
Huwa unafanyaje hili likitokea?
taarifa muhimu
Sehemu ya juu ya fomu ya rufaa ina taarifa muhimu kwa mtumiaji anayetoa rufaa kuhusu viatu vigumu vinavyoweza kuvuliwa, yaweza kutumika au kutokutumika.
Mtoa rufaa hutumia taairfa hii ili kuhakikisha kuwa kiatu kigumu saidizi kinafaa.

Swali
angalia fomu ya rufaa na usome taarifa kwa Madaktari wanaotoa rufaa.
Ni sababu zipi kati ya hizi zifuatazo mhitaji anapaswa kupewa rufaa kwenda kupata viatu vigumu saidizi?
Sahihi.
mtu hapaswi kupewa rufaa kama amevunjika mifupa na bado kidonda hakijatengamaa.
Kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa hakiwezi Kutoa Msaada tosha kwa mtumiaji mwenye mifupa iliyovunjika ambayo bado haijatengamaa.
Pia kuna hatari kwa mtumiaji anaweza kuvua kiatu kigumu saidizi na hivi kufanya kidonda kuwa na hali mbaya zaidi.
Sio sahihi.
Mhitaji anaweza kupewa rufaa kwenda kupewa kiati kigumu kinachoweza kuvuliwa kama wana jeraha ambalo limetengamaa kwenye kifundo cha mguu au kidole cha mguuni.
Sahihi.
mtu hapaswi kupewa rufaa iwapo miguu yote miwili imejeruhiwa. ATAPata changamoto kwenye kutembea na anapaswa kwenda kwenye huduma ya kutengamaa. Kiti saidizi cha magurudumu maNne kinahitajika ili kumhamisha kutoka eneo moja kwenda eneo lingine.
Sio sahihi.
mtu mweye jeraha kwenye sehemu laini ya mwili, anaweza kupata rufaa kwenda kupewa kiatu kigumu saidizi
Sahihi.
Ikiwa jeraha la mtu linapaswa kusaidiwa kubaki kwenye nyuzi 90 ili liweze kupona vizuri, huyo mhusika anapaswa kupewa rufaa kwenda kwenye huduma ya mazoezi ya viungo ili ili aweze kutengenezewa kifaa saidizi kigumu kifaa kingine mbadala
Swali
Je, kauli hii ni ya kweli au sio ya kweli?
Fomu hii ya rufaa haipaswi kutumiwa na mtu mwenye kidonda kwenye sehemu ya kutembelea ya mguu ambacho kinahusiana na ugonjwa wa kisukari.
uko sahihi Ikiwa umechagua "kweli"
kama mtu ana majeraha ya mguu Yanayotokana na ugonjwa wa kisukari, anapaswa kupewa rufaa kwenda kupata huduma ya matibabu ya vidonda.
taarifa kuhusu mtoa rufaa, mhitaji na hali yake
Ni muhimu habari kuwa imekamilika Wakati wa kupokea rufaa yoyote
angalia kama habari imekamilika kuhusu mtoa rufaa, mhitaji na tatizo lake - pamoja na aina na eneo la aliloumia au amaposikia Maumivu.

Maelekezo ya matumizi
Sehemu ya mwisho kwenye fomu ya rufaa hutoa melekezo ya mtoa rufaa ya namna ambavyo mtu anapaswa kutumia kiatu kigumu saidizi chake huku jeraha lake likiendelea kupona.
taarifa hii inajumuisha:

Kubeba uzito
Hii inahusu uzito ambao mtumiaji wa kiatu kigumu kisaidizi anaweza kubeba kwenye kiatu hicho.

Kutokubeba uzito
mtumiaji wa kiatu kigumu saidizi hapaswi kubeba uzito wowote kwenye kiatu.

Ubebaji wa uzito kiasi
mtu anaweza kubeba uzito kwenye mguu na kiatu kigumu saidizi

Ubebaji wa uzito kamili
mtu anaweza kubeba uzito kamili kwa miguu yote miwili.

Utaratibu wa kawaida wa uvaaji
Unaelezea kama mtu anaweza kuvua viatu vigumu saidizi muda wowote, kwa mafno wakati anapoenda kuoga au kulala.


UnamKumbuka Jess?
Jess alipewa ruhusa ya kuvua kiatu kigumu saidizi Wakati wa anapooga lakini sio wakati anapolala.
Urefu wa muda wa matumizi
Muelekeze muda ambao mtumiaji anahitaji kuvaa kiatu kigumu saidizi.


UnamKumbuka Wei?
Wei alipata jeraha sehemu laini ya mwili baada ya kucheza mpira wa kikapu.
Daktari amemtaka Wei kuvaa kiatu kigumu saidizi chake kwa walau wiki sita wakati jeraha lake likipona.
Utajifunza zaidi kuhusu maelekezo ya matumizi katika Somo la Tatu.
Fanya tathmini
Huu ni muda ambao daktari angependa kumuona mgonjwa kwa ajili ya kutathmini jeraha lake.

Swali

Daktari amejaza fomu ya rufaa ya Mario. angalia fomu na jibu maswalifuatayo hapa chini.

1. Ni mguu gani wa Mario ambao unahabaritaji kiatu kigumu saidizi ?
uko sahihi iwapo ukichagua mguu wa kulia.
katika fomu ya rufaa, daktari ameweka alama ya vema kwenye mguu ambao una kidonda kifundo cha mguu wa kulia.
2. Kubeba uzito: Mario anaweza kubeba uzito kiasi gani kwa kupitia kiatu kigumu saidizi ambacho amekivaa?
Umepatia iwapo umechagua c kama jibu
3. Utaratibu wa kawaida wa uvaaji: Je, Mario anaweza kuvua kabisa kiatu kigumu saidizi chake?
uko sahihi iwapo umechagua jibu kuwa ni "a".
Mario anaweza kukivua wakati anapoenda kuoga au kulala.
4. Muda wa matumizi: Hakuna tarehe ya ukaguzi au muda wa matumizi kwenye fomu ya Mario. Utafanya nini?
uko sahihi iwapo umechagua jibu kuwa ni "a".
Wasiliana na mtu aliyetoa rufaa ili kujua muda ambao Mario anahitaji kutumia kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa.
b na c sio sahihi.
Mario anaweza kuwa hana shida yoyote Wakati wa kuvua kiatu kigumu lakini huenda kidonda chake kisipone vizuri. Hali ya kidonda chake inaweza kuwa mbaya zaidi Ikiwa haTatumia kiatu kigumu kinachoweza kuvuliwa