Vifaa saidizi vya Kujitunza zilivyojumuishwa kwenye TAP
Moduli za TAP zinajumuisha vifaa saidizi vinavyotumika Mara kwa mara pamoja na:
- Viti saidizi vya bafuni
- Viti saidizi vya msalani
- Bidhaa za kufyonza vimiminika
- Katheta
- Vifaa saidizi vya kuvaa nguo
- Vifaa saidizi vya Kula na kunywa.
Soma kuhusu utangulizi mfupi wa bidhaa hizi.
Viti saidizi vya bafuni
Viti saidizi vya bafuni huwekwa bafuni au eneo ambalo mtumiaji anakaa wakati anapojiogesha.
Viti saidizi vya bafuni ni muhimu kwa watu ambao hawawezi kusimama na / au kusimama vizuri bila kuyumba Wakati wa kuoga.
UnamKumbuka Petro?
Ana jeraha kwenye uti wa mgongo na amepooza chini ya Kiuno chake. Anatumia Kiti saidizi cha magurudumu kuzunguka hapa na pale. Petro ana kiti saidizi cha bafuni katika bafu yake. Anaweza kuhama mwenyewe kutoka kwenye bafu hadi kwenye kiti saidizi cha kuoga. Kisha anasukuma Kiti saidizi cha magurudumu mbali na njia ya Maji, na kuoga mwenyewe.
Viti saidizi vya kuoga vyenye magurudumu ni muhimu kwa watu ambao wanahitaji kukaa Wakati wa kuoga na na wanaopata taabu kuingia na kutoka bafuni.
UnamKumbuka Ronin?
Wakati mguu wake na mkono wake vikiendelea kupona baada ya Kupata ajali, atakuwa akitumia kiti saidizi cha bafuni chenye magurudumu. Kiti kinawekwa karibu na kitanda chake, na wazazi wake wanamsaidia kukaa (kuhamia\) juu yake. Kisha anasukumwa hadi bafuni Wakati wa kwenye kiti, ambapo anasaidiwa kuoga.
Kwa habari zaidi kuhusu viti saidizi vya bafuni na namna ya kuvigawa kwa wahitaji, soma zaidi moduli ya Viti saidizi vya bafuni na msalani.
Viti saidizi vya msalani
Viti saidizi vya msalani vina sehemu ya kukaa ambayo inaweza kuondolewa, sehemu ya kupumzisha mkono na ndoo inayohamishika. Vingine vina sehemu ya kuegemea.
Vinaweza kutumika pia:
- Juu ya choo (bila ya kutumia ndoo inayohamishika\) au bila kuwa na choo
- katika sehemu yoyote faragha (na ndoo inayohamishika\).
Viti saidizi vya choo hutoa Msaada zaidi Wakati wa kukaa na kusimama kuliko Msaada vinaoutoa msalani
Baadhi ya viti saidizi vya msalani vina magurudumu.
Viti saidizi vya choo vinaweza kuwa na manufaa kwa watu ambao:
- Wanapata taabu kuingia na/au kutoka msalani
- Wanapata taabu kukaa juu ya choo na kutoka kwenye choo
- Wanahitaji Msaada kukaa vizuri Wakati wa kujifunza au kujifunza kwa mara nyingi kuhusu stadi za kutumia choo (mafunzo ya kutumia choo).
Je, unamKumbuka Aida?
Baada ya kupata ugonjwa wa kiharusi ; Aida alianza kuingia msalani kwa taabu. Alipata taabu zaidi kwenye kukaa chini na kusimama.
Sasa anatumia kiti saidizi cha msalani na ndoo inayohamishika.
Wakati wa mchana; ndoo huondolewa na kiti huwekwa juu ya choo.
Kukaa na kutoka kwenye choo ni mambo rahisi kwa Aida kwa vile kiti saidizi cha msalani kina sehemu ya kuweka mkono ambayo anaweza kushikiria.Binti yake anamsaidia kutembea kwenda msalani na kutoka msalani
Kiti saidizi cha msalani pamoja na ndoo vinawekwa karibu na kitanda cha Aida
Anaweza kwenda kwenye kiti saidizi chake mwenyewe bila ya kuhitaji Msaada kutoka kwa binti yake Wakati wa uSiku. Ndoo husafishwa asubuhi.
Ili kupata taarifa zaidi kuhusu viti saidizi vya msalani na namna ya kuvigawa kwa wahitaji, soma na maliza moduli ya TAP kuhusu viti saidizi vya bafuni na msalani.
Bidhaa za kufyonza vimiminika
Bidhaa zinazonyonya Maji ambazo zimezungumziwa kwenye TAP ni zile ambazo huvAliwa na mtu. Bidhaa hizi ni kama vile:
- Ziko katika maumbo na ukubwa tofauti
- Zinaweza kutumiwa na wavulana, wasichana, wanaume na wanawake
- Ni pamoja na bidhaa zinazofaa pale kunapokuwa na Kutokwa kwa mikojo kwa kiwango cha kidogo, cha kati na kikubwa.
- Zinaweza kusafishwa kwa kuoshwa na kutumika kwa mara nyingine tena au kutumika mara moja na hogo mbali (matumizi ya mara moja\).
Bidhaa za zinazonyonya maji zinaweza kuwa na manufaa kwa watu ambao wanapata usumbufu wa kuzuia na kuruhusu haja ndogo. Zinaweza kunyonya mkojo na/au kinyesi na kusaidia kulinda ngozi na mavazi ya mhusikamiaji; kuwawezesha kuendelea na maisha yao ya kawaida ya kila siku.
UnamKumbuka Aleisha?
Aleisha ana ugonjwa wa mtindio wa ubongo na anapata taabu kuratibu na kudhibiti kuhama kwake kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kwa kawaida anaweza kuhisi pale anapohitaji kwenda msalani, na mama yake anamsaidia kufika huko na kutumia choo.
Hata hivyo, wakati mwingine hawezi kudhibiti kibofu chake cha Mkojo na haja kubwa. Wakati Aleisha anapokuwa shuleni anavaa Bidhaa za kufyonza kimiminika ambazo anaweza kuvua bila usumbufu. Bidhaa hizi husaidia kuweza kudhibiti kibofu chake cha Mkojo au Kutokwa kwa haja kubwa.
Ili kupata habari zaidi kuhusu bidhaa zinazonyonya Maji, na namna ya kuzigawa soma na maliza moduli ya bidhaa zinazonyonya Maji za TAP
Katheta
Katheta ni mrija laini ambao huondoa Mkojo kutoka kwenye kibofu cha Mkojo cha mgonjwa.
Katheta zinaweza kuwa na manufaa kwa watu ambao wana shida kutoa Mkojo kutoka kwenye vibofu vyao vya Mkojo.
Kuna aina mbili kuu za Katheta:
- Katheta zinazochomekwa na kuchomolewa Mara kwa mara ( zinajulikana pia kama Katheta za nelaton)
- Katheta zinazochomekwa na kukaa kwa Muda mrefu (pia huitwa Katheta aina ya Foley)
Katheta zinazochomekwa na kutotolewa Mara kwa mara ( Katheta aina ya nelaton)
Katheta za Nelaton huingizwa kwenye kibofu cha Mkojo ili kuondoa Mkojo na kisha kuondolewa.
Hii inafanywa kwa Siku nzima, wakati mtumiaji anapohitaji kutoa Mkojo kwenye kibofu.
Ili kutoa Mkojo ulio katika kibofu chake , Petro anatumia katheta ya inayochomekwa na kuondolewa baada ya kutoa Mkojo wote ulio kwenye kibofu.Kwa kila Siku, Petro anatumia katheta kutoa Mkojo kutoka kibofu chake na kuumwagia msalani.. Kazi hii anaifanya Mara kwa mara.
Katheta zinazochomekwa na kukaa kwa Muda mrefu (pia huitwa Katheta aina ya Foley)
Zinaingizw katika kibofu cha Mkojo na kubaki ndani kwa uda wa wiki kumi na mbili. Katheta huondoa Mkojo na kuuweka kwenye mfuko maalum wa kukusanya Mkojo. Mfuko huu husafishwa kila mara.
Katheta zinaingizwa ndani kuptika sehemu ya Mkojo zinaweza kutumika kuwasaidia watu ambao wanatokwa Mkojo kwa taabu kama vifaa saidizi za kufyonza kimiminika Mkojo hazifai kutumika kulingana na hali ya mgonjwa.
Kutana na Maria
Maria ana ugonjwa wa neva (sclerosis). Huu ni ugonjwa unaoathiri sehemu ya juu ya Hisia za Kusikia na Kuona ya.kwenye ubongo na uti wa mgongo. Anatumia Kiti saidizi cha magurudumu kutoka eneo moja hadi jingine, na anaweza kutumia mikono yake kwa nadra. Maria ana mtoa huduma anayemsaidia katika Kujitunza
Maria anahitaji katheta ili imsaidie kutoa Mkojo kutoka katika kibofu chake. Amechagua kutumia katheta inayowekwa kwenye kibofu cha mtumiaji na kukaa huko kwa Muda mrefu.
Ala (uridome)
Ala ni chaguo jingine (Bidhaa za kufyonza kimiminika Maji) ambalo wanaume wanaweza kutumia kwenye kukabili Kutokwa kwa Mkojo. Wanavalisha uume wao ala ( mfuko kama kondomu) na kuunganisha na mpira laini. Mpira huu laini unaunganishwa na mfuko maalum wa kukusanya Mkojo
Ili kupata habari zaidi kuhusu Aina tofauti za katheta na mambo ya kuzingatia kuhusu ugawaji wake kwa wahitaji, soma na maliza moduli inayohusu katheta iliyo kwenye TAP.
Vifaa saidizi vya kuwezesha kuvaa nguo
Fimbo ya kukusaidia kuvaa nguo
Fimbo ya kuvaAlia nguo ina ndoano yenye umbo la 'c' kwa upande mmoja, na ndoano ya 's' iliyo upande mwingine.
Hutumika kusaidia kuvaa na kuvua nguo ndani .
Fimbo za kuvalia nguo zinaweza kuwafaa watu ambao hawawezi kuinama kwa urahisi kwenda Wakati wa na inaweza kuwafaa wahitaji ambao wanaoweza kuzungusha mkono au mikono kwa kiasi kidogo.
Kifaa saidizi cha kuvalia Viatu
Hiki ni kifaa cha kuvalia Viatu chenye mkono mrefu, ili kumsaidia mvaaji kuweza kuweka mguu wake kwenye kiatu
Hii inaweza kuwanufAISHA watu ambao hawawezi kuegemea kwa Wakati wa kwa urahisi, au wale ambao wanaweza kusogeza mikono au miguu yao kwa taabu.
Kifaa saidizi cha kuvaa soksi
Kifaa saidizi cha kuvaa soksi ni kipande cha plastiki rahisi chenye kamba mbili zilizounganishwa sehemu ya mwisho. Soksi fupi na socks ndefu zinaninginizwa kwenye plastiki, halafu mtumiaji anaweka mguu wake kwenye soksi kwa kutumia kifaa saidizi cha kuvaa soksi kuvuta soksi yake juu kwa kutumia kamba mbili.
Kifaa saidizi cha kuvalia soksi kinaweza kuwafaa watu wanaovaa soksi fupi au soksi ndefu kwa taabu. Hasa wale ambao hawawezi kuinama kwa Wakati wa au wana weza kusogeza mikono yao kwa taabu.
Je, unamKumbuka Aida?
Aida anavaa nguo zake kwa taabu tangu apate ugonjwa wa kiharusi . Hata hivyo, ameanza kutumia fimbo ya kumsaidia kuvaa nguo. Aidha anatumia kifaa saidizi cha kuvaa soksi na kifaa saidizi cha kuvaa Viatu.Uwepo wa vifaa saidizi hivi, unamaanisha kuwa anaweza kujitegemea kwenye kuvaa
Kifaa cha kuchomeka vifungo vya nguo kwenye matundu yake na kuvuta cha zipu
Kifaa cha kuvAlisha vifungo vya nguo na kuvuta kichwa cha zipu kina umbo la 'c' sehemu ya mwisho ili kuweza kuvuta zipu na ndoano ya umbo la Almasi upande mwingine ili kuweza kuingiza vifungo vya nguo kwenye matundu yake.
Kinaweza kuwasaidia watu ambao wana shida katika kusogeza mikono yao
UnamKumbuka Samweli?
Samweli anapata taabu katika kufanya kazi ndogo ndogo. Kazi hizi ni kama vile kufunga vifungo vya nguo na kufunga kamba za Viatu. Anatumia kifaa cha kuchomeka vifungo kwenye matundu yake na kuvuta zipu ili aweze kupata urahisi katika kuvaa nguo
Pia anatumia Viatu ambavyo vina Velcro badala ya vile vyenye kamba kwa vile anavimudu kwa urahisi sana.
Vifaa saidizi vya Kujitunza vinavyosaidia kwenye Kula na kunywa
Vifaa vya mezani ambavyo vimebadilishwa kwendana na mtumiaji
Vifaa saidizi vya kula kama vile visu, uma, vijiko na njiti vinaweza kubadilishwa ili kuweza kushikiliwa kwa urahisi
Ni rahisi kwa watu wenye Uwezo mdogo wa kusogeza mikono na ambao ni dhaifu; kuweza kushikilia vifaa vya kulia ambavyo vina sehemu za kushikilia pana.
Kitanzi laini au thabiti kinaweza kuongezwa ambacho kinashikilia kifaa saidizi cha kulia kwenye mkono wa mtumiajimiaji. Hii ni muhimu kwa watu ambao hawawezi kushikilia vyombo lakini wanaweza kusogeza mkono na wanaweza kudhibiti mkono wao.
Sahani zilizowekewa kingo ya ziada na sahani/bakuli ambazo zimebadilishwa
Sahani zilizowekewa kingo ya ziada ni sahani zenye kipande cha nusu-mviringo cha plastiki ambacho kinatokeza upande wa sahani.
Sahani zilizobadilishwa au bakuli zina kifaa ambacho 'kimetengenezwa ndani yake' - sehemu moja ya sahani au bakuli imeinuliwa.
Sahani zilizowekewa kingo ya ziada na sahani/bakuli ambazo zimebadilishwa ni muhimu kwa watu ambao wanaweza kutumia mkono mMoja tu kula, kwani husaidia kuchukua chakula au 'kukiweka' kwenye uma, kijiko au vyombo vingine vya kulia chakula.
Vikombe vilivyobadilishwa
Vikombe vilivyobadilishwa vinaweza kuwa na mikono kurahisisha kushikika kwake / au kifuniko cha shimo ndogo ili kuruhusu kunywa kwa urahisi bila kumwagika.
Vikombe vilivyobadilishwa vinaweza kuwa na manufaa kwa watu ambao wana Uwezo mdogo wa kuhamisha mkono kutoka sehemu moja kwenda nyingine na mawasiliano duni ya kimwili
UnamKumbuka Aleisha?
Aleisha anapata taabu kuratibu na kudhibiti kuzunguka kwake kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Anatumia kikombe kilichobadilishwa chenye sehemu mbili za kushikia na mfuniko ambao unaweza kushikika na kuzuia kilichomo kumwagika
Pia anatumia kijiko chenye sehemu nene ya kshikilia pamoja na kitanzi ambacho kinamsaidia kushikilia kikombe