Kutumia kiti saidizi cha msalani na bafuni kwa mafanikio
Watu wengine wanaotumia kiti saidizi cha msalani wanaweza kupata kwenye kudhibiti Mkojo na haja kubwa.
Ikiwa hawawezi kufika msalani kwa haraka inavyopaswa, wanaweza kutokwa na Mkojo.
Je, unamKumbuka Aida?
Ameweka kiti saidi chake cha msalani karibu na kitanda chake ili aweze kukifikia kwa haraka uSiku. Hii inamsaidia kuepuka Kupata ajali.
Hapa chini kuna baadhi ya njia ambazo zinaweza kumsaidia mtu kufika kwenye kiti saidizi chake na kuepuka kutokwa na Mkojo (Kutokwa\):
- Hakikisha choo kiko karibu na kinafikika kwa urahisi
- Kuboresha Uwezo wako wa kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kwa kutumia vifaa saidizi vya kuhama
- Omba Msaada kutoka kwa wanafamilia na wanahudumu kufika msalani kwa wakati
- Chagua nguo ambazo zinavaliwa na kuvuliwa kwa urahisi
- Ikiwa mtumiaji anachanganya kuhusu choo cha kutumia, weka alama na picha kwenye mlango wa choo,inayoonyesha mahali anapoweza kuingia.
- Tumia choo Mara kwa mara baada ya kunywa na kula. Au tenga muda wa KuKumbuka kwenda msalani Kila baada ya vipindi vya kawaida
- Ili kujisadia vizuri, tenga muda wa kutosha wa kuwa kwenye choo
- Tumia nguo za kufyonza ili ziweze kukusaidia ikiwa utatokwa na haja.
Swali
UnamKumbuka Mzee Mathias?
Mathias ana ugonjwa wa kisukari na ni dhaifu. Alikuwa anaishi na mkewe. Wakati mwingine hufika msalani lakini hawezi kuvua nguo zake kwa wakati na Mkojo kuanza kutoka. Hili jambo huwa linamsikitisha sana.
Ni nini kinaweza kusaidia Mathias kutokukwa na Mkojo kwa bahati mbaya?
- Mathias anaweza kuvaa suruali ambazo anaweza kuzivua kwa urahisi na kwa haraka
- Mathias anaweza kwenda msalani mapema, kwa mfano mara tu baada ya kunywa kinywaji.
- Mathias anaweza kufaidika na kuvaa nguo za kufyonza Maji wakati anapotoka nyumbani ili ziweze kumsaidia pale itakapotokea.
Kutana na Luciana na mumewe Jose
Luciana ana umri wa miaka 73 na anaishi na mumewe Jose nyumbani kwao. Luciana ana shida ya KuKumbuka na kupanga shughuli zake. Pia ana ugonjwa wa Maumivu kwenye maungio na anatembea kwa kutumia rolata. Anatumia kiti saidizi cha msalani ili iwe rahisi kukaa na kusimama.
Wakati mwingine Luciana anasahau kwenda msalani. Wakati anapoKumbuka kufanya hivyo, anakuwa hawezi kufika msalani kwa haraka inavyopaswa. Hali hii inawasikitisha sana Luciana na Jose.
Ni nini kinaweza kumsaidia Luciana kuepuka ajali?
- Kulingana na umbali uliopo hadi kufika msalani, sogeza kiti saidizi cha msalani hadi mahali pa faragha ambapo Luciana hupumzika. Ndoo inayoweza kuhamishwa itahitajika kwa ajili ya kiti saidizi hiki.
- Jose angeweza kumkumbusha Luciana kwenda msalani, kwa mfano kwenda huko Kila baada ya masaa mawili.
Baada ya kufundisha watumiaji namna ya kutumia kiti saidizi cha msalani au bafuni, ni muhimu pia kuwafundisha namna ya kukitunza. Mada inayofuata inatoa taarifa kuhusu namna ya kusafisha kiti saidizi na kukitunza kitumike kwa Muda mrefu.