Skip to main content
0% Complete
Uwezo wa kusikia

Vifaa saidizi vya kusikia vilivyosetiwa tayari

Moduli hii inatambulisha namna ya kugawa vifaa saidizi vya kusikia. Inatoa mafunzo huduma ya afya ya msingi kwa wafanyakazi wanaotoa huduma kwenye jamii kuhusu namna ya kugawa vifaa saidizi vya kusikia vilivyosetiwa tayari kwa watu wazima kwa kufuata hatua nne za huduma.

Muda wa Moduli: Saa 3.5 mtandaoni, ikifuatiwa na mazoezi yanayosimamiwa.

Kabla ya kuanza kusoma moduli hii, hakikisha kuwa umekamilisha Moduli zifuatazo:

Rasilimali ambazo utahitaji wakati wa upimaji

Kipimo cha kusikia:

  • Vipima sauti na spika za masikioni zinazochuja kelele
  • Chumba chenye utulivu
  • Uteuzi wa vifaa saidizi vya kusikia vilivyosetiwa tayari, Ikiwa ni pamoja vyenye ukubwa tofauti wa vitu vinavyochomekwa kwenye masikio na betri ziada

Ufungaji wa vifaa saidizi vya kusikia:

  • Vifaa saidizi vya kusikia katika ukubwa tofauti
  • Bomba la ziada la kutumia kwenye kifaa saidizi cha kusikia
  • Mikasi
  • Kalamu

Ukaguzi/utunzaji wa vifaa saidizi vya kusikia:

  • Bomba la kutumia kusikiliza (Stetoklipu)
  • Seti ya kusafisha Ikiwa ni pamoja na brashi, waya na nguo
  • Chombo chenye maji ya sabuni na kitambaa cha karatasi kusafisha na kukausha kichwa cha kifaa saidizi cha kusikia
  • Hifadhi ya kifaa saidizi cha kusikia (chombo cha kuondoa unyevu)

Bonyeza kwenye linki iliyo hapa chini ili kuweza kupakua na kuchapa:

Nembo ya Raslimali Rasilimali

Bofya kwenye yafuatayo ili uweze kupakua na kuchapa taarifa zifuatazo: