Viti saidizi vya bafuni
Viti saidizi vya msalani na vigoda huwawezesha watumiaji ambao wana Uwezo mdogo wa kuhama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Aidha, vinawafaa wale wanaoyumba pale wanaposimama, na wale ambao wana mawasiliano hafifu kwenye viungo vyao Wakati wa kukaa na kuoga.
Vinaweza kutumika katika eneo ambalo watu wanatumia kuoga kama bafuni

Kiti saidizi cha bafuni

Kigoda saidizi cha bafuni
Swali
angalia Picha ya kiti saidizi cha bafuni na kigonda saidizi cha bafuni hapo juu. Vifaa saidizi hivi vina tofauti gani kubwa?
Tofauti kubwa ni kwamba kiti saidizi cha bafuni kina sehemu ya kuegemea mgongo na kigoda saidizi cha bafuni hakina
Kiti saidizi cha bafuni kina sehemu ambayomgongo waweza kuegemea; hivyo ni kizuri zaidi kwa mtumiaji mwenyeyumba akisimama; au yule ambaye hana mawasiliano mazuri ya kimwili . Aidha, kinamsaidia mtu mwenyechoka kwa haraka
Kuna aina nyingi za viti na vigoda saidizi vya bafuni.
Kila mara, hakikisha unaangalia sifa muhimu zifuatazo Wakati wa kuchagua kiti saidizi cha bafuni.
Sifa muhimu
Viti na vigoda saidizi vya bafuni vinapaswa kuwa:
- Imara na vinavyodumu
- kutokushika kutu wala kulowana na Maji
- Vimetengenezwa kwa ustadi ili kuweza kuzuia mtumiaji kuumia
- Kuwa na mpira kwenye miguu (isipokuwa kama kina magurudumu)
- Kuwa na breki (ikiwa kina magurudumu, na wala sio miguu)
- Miguu ina urefu ambao unaweza kupunguzwa au kuongezwa
- Vimetengezwa maalum kwa kuweza kubeba uzito wa mtumiajimiaji.
Sifa nyingine
Sifa nyingine ambazo zinaweza kuwa za muhimu hasa hasa kwa watu ambao wanahitaji Msaada ili waweze kusogea kutoka sehemu moja kwenda nyingine:
- Sehemu ya kuegemeza mgongo
- Magurudumu Yanayoweza kuelekea upande tofauti na Yana breki
- Sehemu ya kupumzisha mkono inayoweza kusogezwa Wakati wa na kubadilishwa badilishwa.
- Sehemu ya kuweka miguu yenye urefu ambao unaweza kubadilishwa
- Sehemu ya kuzuia mgandamizo iliyo juu ya kiti, na kwenye sehemu ya kuegemeza mkono na mgongo.
Kazi
angalia kwa umakini viti na vigoda saidizi vya msalani vinavyopatikana kwenye eneo lako la kazi na eneo unaloishi.
- Viti na vigoda vya bafuni vina idadi ipi ya sifa muhimu?
- Je kila kiti saidizi cha bafuni kinapaswa kuwa na sifa zipi muhimu?
- Je, viti saidizi vya bafuni vina sifa zingine ambazo hazijaorodheshwa hapo juu?
Kiti saidizi chenye muunganiko wa kiti saidizi cha bafuni na msalani
Baadhi ya viti vya msalani vimetengenezwa katika namna inayoruhusu kuweza kutumika bafuni pia.
Kiti hiki kinaweza kumsaida sana mtu mwenyehitaji kiti saidizi cha msalani na kile cha bafuni, kwa vile atapata kiti kimoja badala ya kuhitaji viti viwili.
Kiti saidizi cha bafuni na msalani kinachotolewa na mtoa huduma aliyebobea kwenye huduma hiyo
Baadhi ya viti saidizi vya msalani na bafuni vina Msaada mkubwa katika kumfanya mhusikamiaji kuwa katika mkao mzuri. Viti hivi vinahitajiwa na Watoto kwa Watu wazima ambao wanapata taabu kukaa wima.
Moduli hii haitoi mwongozo kuhusu namna ya kugawa viti saidizi vya bafuni na masalani vinavyotolewa kwa ushauri wa mtaalam mbobezi.