Nani anatumia viti saidizi vya msalani na vile vya bafuni?
Watoto, Watu wazima na wazee hutumia Aina tofauti za viti saidizi vya bafuni na msalani kutokana na sababu mbalimbali
Mara nyingi sababu hizi hutokana na:
- Vikwazo vya kimazingira
- Uwezo wa kimwili.
Swali
1.Zifuatazo ni baadHabari ya sababu ambazo zinaweza kumfanya mhusikamiaji kwenda msalani au bafuni kwa taabu.
Chagua vikwazo ambavyo ni vikwazo vya kimazingira
Vikwazo vya kimazingira ni:
- Njia ya msalani au bafuni ni nyembamba, imefungwa, mbaya na ina mwinuko
- Umbali wa kwenda msalani na bafuni ni mrefu sana
- Kuna hatua kadhaa kuelekea msalani na bafuni.
2. Zifuatazo ni baadHabari ya sababu zinazoweza kumfanya mhusikamiaji kwenda msalani au bafuni kwa taabu.
Chagua sababu ambazo zinahusiana na Uwezo wa mtumiaji kukabiliana na mazingira yake.
Sababu za Uwezo wa mwili wake kukabiliana na mazingira yaliyomzunguka:
- Anakaa chini au kuchuchumaa kwa taabu.
- Hawezi kusimama, au anapata shida kusimama kwa usalama.
- Ameanguka zaidi ya mara moja kwa mwaka uliopita au anaogopa kuanguka tena.
Soma baadhi ya mifano ya watu wanaotumia vifaa saidizi hivi na kwanini.
Kutana na Petro
Petro ana jeraha kwenye uti wa mgongo na hawezi kutembea kwa kutumia miguu yake. Anatumia Kiti saidizi cha magurudumu kuzunguka kutoka eneo moja hadi lingine.
Petro anatumia kiti saidizi cha bafuni kwa sababu hawezi kusimama kuoga mwenyewe. Ni rahisi kwenda bafuni kwake. Anaweza kufika huko mwenyewe na kutoka kwenye kiti saidizi chake chenye magurudumu na kukaa kwenye kiti saidizi cha bafuni.
Kutana na Aida
Aida alipata ugonjwa wa kiharusi ambao ulisababisha apate udhaifu upande wake wa kushoto. Anatumia fimbo ya kuteWakati waa ili kuweza kuhama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
Uwezo wake mdogo wa kuhama kutoka eneo moja kwenda lingine kunamaanisha hawezi kusogea kwa haraka vya kutosha kufika msalani pale anapohitaji kufanya hivyo. Pia anapata taabu kukaa na kusimama kutoka choo cha kukaa.
Aida amegundua kuwa kiti saidizi chake cha msalani ambacho kina sehemu ya kuweka mikono kinamsaida. Anatumia sehemu ya kuweka mikono kumsaidia aweze kukaa na kusimama.
Kiti saidizi cha msalani kinawekwa juu ya choo cha kukaa Wakati wa mchana, na binti yake anamsaidia kuweza kufika msalani.
Wakati wa uSiku, kiti saidizi chake cha msalani kinakuwa karibu na kitanda chake. Hii inamrahisishia kwenda msalani mwenyewe bila ya kupata Msaada kutoka kwa mtumiaji mwingine.
Aidha, Aida anatumia kiti saidizi cha bafuni
katika somo linalofuata, utajifunza namna ya kuchagua kiti saidizi cha msalani na kiti saidizi cha bafuni kwa kwendana na mahitaji ya mhusikamiaji.
Umekamilisha Somo la kwanza!
Ikiwa una Maswali au maoni yoyote, Tafadhali yaandike kwenye jukwaa la majadiliano.