Muonekano wa macho yenye afya njema
Kazi
angalia mifano ya macho yaliyoonyeshwa hapa chini,yenye hali nzuri ya afya
Angalia sifa zifuatazo:
- Sehemu Nyeupe ya jicho haina kitu chochote
- Sehemu ya kati ya jicho (mboni) ni inang'ara
- Sehemu ya kati ya jicho (mboni) ni ya mviringo
- Hakuna wekundu au uvimbe kwenye macho
- Macho yote mawili yanaangalia upande mmoja.
Kagua Afya ya macho
Matatizo ya kiafya ya macho Yanaweza kuathiri Uwezo wa mtumiaji kuona (uoni).
Hata hivyo, Matatizo mengi ya afya ya macho Yanaweza kutibiwa na uoni wa mtumiaji kuboreshwa au kurejeshwa kikamilifu.
Kila mara angalia Matatizo yoyote ya kiafya ya macho kabla ya kumpa mgonjwa miwani ya kusomea kwa mhitaji.
Swali
Ni dalili gani zinazoonyesha kwamba mtu ana tatizo la Afya ya macho?
- Wekundu
- Uvimbe
- Uvimbe, uoto juu au karibu na jicho
- Inatokwa na uchafu
- macho kuwa maKavu, au kuwASHA
- Maumivu ya kichwa
Dalili za matatizo ya kiafya ya macho
Maelekezo
Soma orodha ya dalili za kawaida zinazoonekana za shida ya afya ya macho, na angalia picha zinazofanana.
- Katikati ya jicho la mtu ni jeupe au mawingu
Hii ni ishara inayowezekana ya mboni ya jicho. Mboni ya jicho ni ugonwa ambao ni wa kawaida kwa wazee, hata hivyo inaweza pia kuathiri vijana. ugonjwa huu hupunguza kwa kiasi kikubwa uoni wa mtumiaji.
Katarakti zinaweza kutibiwa. Rufaa kwa mtaalamu wa afya ya macho ni muhimu.
- Wekundu au uvimbe mahali popote au karibu na jicho
- Uoto, uvimbe mahali popote au karibu na jicho
- Kutokwa na uchafu kutoka kwenye macho au kope
- Makope ya macho Yana hali ya kusinzia

- jicho moja, au macho yote Yanageuka ndani au nje (squint)

- Kupepesa macho a au macho yako kwenye hali ya kukonyeza
- Mboni (sehemu nyeusi ya jicho) hazibadiliki ukubwa kwa kuendana na Mwanga, ni za ukubwa tofauti, au sio za mviringo
Maelekezo
angalia hii video hii ili uone namna jicho lenye afya linavyobadilika kwa kadiri ya ukali wa Mwanga.
Onyo
Pamoja na dalili za kimwili zilizo hapo juu, kupoteza uwezo wa kuona au maumivu ya kichwa yanayodumu kwa zaidi ya saa chache, yanaweza kuashiria tatizo kubwa la kiafya. Mwone daktari mara moja.
Kisukari na afya ya macho
Kisukari kInaweza kusababisha Kupoteza uwezo wa kuona. Hata hivyo, hii inaweza kuzuiwa kwa kugudundua mapema tatizo na kutoa matibabu sahihi.
Kwa maana hiyo, ni muhimu kumuUliza mgonjwa kama ana ugonjwa wa kisukari.
mtu yeyote mwenye ugonjwa wa kisukari anapaswa:
- Kuwa na mpango wa matibabu na daktari wake au na sehemu anapata matibabu dhidi ya ugonjwa wa kisukari.
- Kuwa na anafanya vipimo vya uoni vya macho yake kwa mtaalamu wa afya ya macho.
Majadiliano
Jadili na Wanafunzi wenzako:
- Kwenye eneo unaloishi; watu wenye ugonjwa wa kisukari hupata wapi matibabu?
- Ni namna gani unawaelekeza watu kwenda kupata hizo huduma ?
Maelekezo
Jifunze zaidi kuhusu afya ya macho na jinsi ya kudhibiti matatizo ya afya ya macho katika kozi ya huduma ya macho ya msingi ya TAP .









