Sasa umekamilisha tathmini na vipimo vyote ili kubaini kama kiatu kinamfaa na kuweza kumpa hicho kiatu.
Unaweza pia kupanga hatua nyingine ambazo utazichukua pamoja na mhusika.

Kugawa viatu tiba

Tumia taarifa kutoka kwenye tathmini ili kutambua kama ni sawa kumpa mhitaji viatu tiba.
kama jibu ni "ndio":
- Gawa viatu tiba ambavyo mvaaji mtarajiwa amechagua
- mpe rufaa kwenda kwenye huduma nyingine
- Kufundisha kuhusu orodha ya vitu vya elimu
- Weka tarehe ambapo utamFuatilia mgonjwa
kama jibu ni hapana:
- mpe rufaa kwenda kwenye huduma nyingine.
Fundisha

Kulingana na tathmini uliyoifanya pamoja na uchaguzi wa viatu aliyoufanya mvaaji mtarajiwa, amua ni kitu gani kitakuwa muhimu kumfundisha kuhusu viatu tiba na utunzaji sahihi wa miguu.
Husisha wanafamilia au mlezi wa mhusika pale utakapoona inapofaa.
Utajifunza zaidi kuhusu nini cha kumfundisha mhuska katika Somo linalofuata.
Toa rufaa

rufaa kwenda kwenye huduma nyingine inaweza kuhitajika.
angalia sehemu ya nyuma ya fomu ili kujua kama kulikuwa na ushauri wa rufaa kutoka kwenye sehemu mojawapo kati ya tathmini au mchakato wa kutafuta kipimo sahihi.
Utunzaji wa kidonda / kliniki ya mguu
Weka alama kama mhusika anahitaji:
- Utunzaji wa kidonda
- Tathmini zaida ili kujua kama ana hatari ya wastani au kubwa ya kupata kidonda.
Viungo bandia na vifaa saidizi vya kuvaa mguuni
mpe rufaa kwenye tathmini ya kupewa viungo bandia au vifaa saidizi vya kuvalia viatu kama mhitaji :
- Amekatwa Linki mojawapo lakini hana Linki bandia
- Ana miguu haiwezi kutumia viatu tiba.
- Historia ya kidonda na kukatwa Linki.
Kifaa saidizi
vifaa saidizi ni pamoja na vifaa saidizi vya uoni, Uwezo wa kuhama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine au Kujitunza
Nyingine
kama mhitaji anaonyesha anaweza kufaidika kutokana na rufaa, andika kwamba:
Majadiliano
Na mwenzio, linganisha mawazo yako na maswaliliyo kwenye Fomu ya tathmini ya viatu tiba vya TAP.
Mfano wa mambo Yanayoweza kuzungumziwa ni pamoja na:
- Je ni sehemu gani za tathmini ambazo una uzoefu nazo?
- Ni sehemu gani ya tathmini ambayo ni mpya kwako?
- Je, mambo yaliyo kwenye fomu Yanaeleweka au taarifa zaidi zinahitajika?
- Unadhani itakuchukua muda gani kufanya tathmini kwa kutumia fomu?
Ufuatiliaji
ufuatiliaji ni muhimu kuhakikisha kuwa viatu tiba vinamtosha vizuri mvaaji na vinakidhi mahitaji ya mhusikamiajimiaji.
Kubalianeni tarehe ya kuonana tena kwa ajili ya ufuatiliaji.
- Wiki moja
- Mwezi mmoja.
Pia wanapaswa kufuatiliwa Kila baada ya miezi 12 baada ya kwenda kuonwa kwa mara ya pili.
Utajifunza zaidi kuhusu ufuatiliaji katika somo la nne.