miwani ya kusomea inaweza kuvaliwa Wakati wowote pale mtu anapohitaji kuona kitu kilicho karibu.
Pamoja na kuvaa miwani ya kusomea, wahimize watu kuhakikisha wana mwanga wa kutosha wanapotazama vitu kwa karibu. Pendekeza kwamba:
- Aepuke Kusoma au kufanya kazi zingine katika maeneo yenye Mwanga hafifu
- Atumie vizuri Mwanga wa asili - kwa mfano kaa nje au karibu na dirisha wakati unapofanya kazi kwa karibu.
- Elekeza taa katika kazi zilizo karibu

UnamKumbuka Malik?
Mwajiri wa Malik aliweka taa za ziada kwa juu kwenye vituo vyenye mashine za kushona ili kuwasaidia wafanyakazi kuona vizuri.
Watu wengine wanaweza kuwa na wasiwasi kwamba miwani ya kusomea itayafanya acho yao kuwa na uvivu wa Kusoma. Wahakikishie watu kwamba kuvaa miwani ya kusomea haitawasababisha wavaaji madhara yoyote.
Hata hivyo, Ikiwa mtu aTAPatwa na mojawapo ya matatizo yafuatayo, anapaswa kurudi kwa miadi ya kufuatilia au kuonana na mtaalamu wa afya ya macho:
- Maumivu ya kichwa
- Anaona vitu vya karibu kwa taabu
- Anatumia nguvu sana kuweza kuona kitu
- Wanahitaji kushikilia vitu karibu sana au mbali sana ili kuviona vizuri