Watu wanaweza kupata taabu kutembea kutoka eneo moja hadi lingine kutokana na sababu nyingi.
Baadhi ya Sababu zilizozoeleka zimeelezwa hapa chini.
Udhaifu
mtu ambaye ni dhaifu anaweza kupata taabu kusimama bila ya kuanguka na kuzunguka kutoka eneo moja kwenda eneo lingine.
Maumivu au Kutokunyambulika
Maumivu au kutokunyambulika vinaweza kupunguza Uwezo wa mtumiaji kuzunguka kutoka eneo moja hadi lingine.
Kwa mfano Maumivu kwenye maungio (Maumivu kwenye maungio) Yanaweza kumzuia mtu kuweza kusimama au kutembea.

Kutana na Cali
Cali ni dhaifu na ana ugonjwa wa Maumivu kwenye maungio. Mara nyingi hupata Maumivu kwenye nyonga yake na magoti na hivi kutembea kwa taabu.
Kupooza
Kupooza ni ukosefu wa Uwezo wa kutoa mwili kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Kwa mfano, watu walio na jeraha la uti wa mgongo mara nyingi hupooza miguu. mtu mwenye miguu iliyopooza hawezi kusimama wala kutembea.

UnamKumbuka Petro?
Petro ana jeraha la uti wa mgongo na amepooza sehemu ya chini ya Kiuno chake. Petro ana tatizo la kudumu la uhamaji , kwani hataweza kuzunguka tena bila kuwa na Msaada wa ziada.
Kukatwa mkono au mguu
Watu ambao wamekatwa mguu au miguu wanaweza kutumia vifaa saidizi vya uhamaji kuzunguka kutoka eneo moja kwenda lingine.

UnamKumbuka Asif?
Asif amekatwa mguu chini ya goti
Kusimama bila kuanguka na Mawasiliano kati ya viungo vya mwili
Watu ambao husimama kwa taabu au wana masiliano hafifu ya viungo vyao wanaweza kuzunguka kutoka eneo moja kwenda lingine kwa taabu. Wanaweza pia kuwa katika hatari ya kuanguka. WanASHAuriwa kuvaa viatu vinavyofaa ili kupunguza hatari ya kuanguka.
Watu ambao wanasimama kwa taabu na wenye Mawasiliano hafifu ya viungo vyao, hawawezi kukaa kwa wima wala kuzunguka kutoka eneo moja kwenda lingine bila ya kuwa na Msaada

Kutana na Aleisha
Aleisha ana ugonjwa wa kupooza ubongo na anaona ni vigumu kuratibu na kudhibiti mienendo yake. Anahitaji msaada wa kuzunguka.
Utajifunza zaidi kuhusu viatu vinavyofaa katika Somo la Tatu.
Matatizo ya hisia (hisia\)
Matatizo ya hisia katika miguu au miguu ya mhusikamiaji Yanaweza kupunguza Uwezo wa kuhama na kuongeza hatari ya kuanguka.
mtu mwenye Matatizo ya hisia miguuni mwake pia yuko katika hatari ya kuumia na/au kupata kidonda cha mguuni.
Katika mada inayofuata uTAPata habari zaidi kuhusu kidonda cha mguuni.
Daima himiza mtu yeyote na Matatizo na hisia kuvaa viatu vinavyofaa miguuni kwake.

UnamKumbuka Mzee Mathias?
Mathias ni dhaifu na ana matatizo ya hisia miguuni mwake kutokana na ugonjwa wa kisukari. Anatumia rolata ili aweze kutembea salama.
Kuwa na Uwezo wa kusogea kutoka eneo moja hadi sehemu nyingine kadri inavyowezekana ni muhimu sana kwa afya bora, kujumuishwa na kushiriki kwenye shughuli za kijamii.
Watu ambao wana shida za kuhama kutoka eneo moja kwenda lingine wanaweza kuongezewa Uwezo wa kuhama Wakati wana:
- vifaa saidizi sahihi vya uhamaji
- Ukarabati (Ikiwa inahitajika\)
- mazingira Yanayofikika.
Tazama video hii fupi ili kumsikia Roberto akieleza maana ya kuwa na Uwezo wa kuhama kutoka eneo moja kwenda lingine unavyomaanisha kwake.