Ruka hadi kwa yaliyomo kuu
Uhamaji

Vidonda vya kwenye mguu

Somo: la 1 kati ya masomo 4
Mada: 3 kati ya Mada 3
0% Imekamilika

Mwanamke mwenye bandeji kwenye mguu anatembea kwa kutumia Magongo aina ya Axilla.

Kidonda cha mguuni ni kuharibika kwa ngozi mahali popote kwenye mguu.

Hali hii inaweza kusababishwa na:

  • Kidonda cha kwenye mguu, kwa mfano linaloweza kutokana na kukanyaga kwenye kitu chenye ncha kali
  • Shinikizo au kusugua, kwa mfano kutokana na kiatu kisichokaa vizuri kwenye mguu.

Kidonda cha mguuni kInaweza kusababisha Kupoteza uwezo wa kusogea kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Kidonda chenye maambuzi chaweza kusababisha kukatwa kwa mguu au kifo kabisa.

Majadiliano

Inakadiriwa kuwa duniani kote, kila Sekunde 30, mtu anakatwa mguu kutokana na jeraha la mguu lililosababishwa na ugonjwa wa kisukari.

  • Je, unajua mtu yeyote mwenye kidonda kwenye mguu?
  • Unajua namna kidonda hicho kilivyoaanza?
  • namna ya kukihudumia?
  • Je, kilipona, au kilisababisha Matatizo zaidi?

Kukatwa mguu au mkono mara nyingi Kunaweza kuepukwa kwa:

  • Kuzuia vidonda vya mguuni au
  • Kutambua na kumtibu mtu mwenye vidonda vya kwenye mguu mara tu vinapotokea.

Soma zaidi ili kujifunza zaidi kuhusu kinachosababisha vidonda vya mguuni, na nani ambaye yuko kwenye hatari zaidi ya kupata vidonda vikubwa vya mguuni.

Vidonda vya mguuni Yanaweza kuwa tatizo kubwa kwa watu ambao wana matatizo mengine yoyote ya kiafya kama haya yafuatayo:

Matatizo ya hisia (hisia\) katika miguu

Matatizo ya hisia katika miguu inamaanisha kwamba mtu hawezi kuhisi Maumivu, mgandamizo, joto au anapoguswa.

mtu mwenye Matatizo ya hisia, au hana hisia katika miguu yake yuko katika hatari kubwa ya kupata vidonda vya miguuni, kwa sababu hahisi chochote wakati kitu chochote kinapoudhuru mguu wake.

Watu wenye ugonjwa wa kisukari, ukoma, jeraha la uti wa mgongo au ugonjwa wa kiharusi mara nyingi hupoteza hisia katika miguu yao, na hivyo wako katika hatari ya kupata kidonda cha mguuni.

Watu wengine ambao wanakunywa kiasi kikubwa cha Pombe pia wanaweza kuanza kupoteza hisia katika miguu yao na kuwa katika hatari ya kupata kidonda.

Kwa mtumiaji yeyote mwenye Matatizo ya kuhisi katika miguu yake, kutembea bila ya kuvaa viatu huongeza hatari ya kuumia na uwezekano wa kupata kidonda mguuni.

Josephina na kijana mdogo wanatemea kwenye Maji ya baridi. Wamebeba fimbo ndefu kwenye mabega yao, na samaki wakubwa wakining'inia katika yao.

Swali

Josephina ana umri wa miaka 45, na ana ugonjwa wa kisukari. Hana hisia kamili katika miguu yake na mzunguko wa damu umepungua sana kwenye miguu

Josephina ni mvuvi na hutumia muda mwingi ufukweni na kwenye mashua. Mara nyingi hukaa bila ya kuvaa viatu.

Je, Josephina yuko katika hatari ya kupata jeraha la mguu?



Ndio, Josephina yuko katika hatari ya wastani kwa sababu hawezi kuhisi kikamilifu miguu yake na hajavaa viatu. Anaweza kujeruhi mguu wake Wakati wa ufukweni, ndani ya Maji au kwenye mashua yake. Kupungua kwa mzunguko wa damu huongeza hatari ya kupona kwa taratibu sana na kupata maambukizi.

Kupunguza kwa mzunguko wa damu

Wakati kunapokuwepo mzunguko mdogo wa damu kwenye miguu, kidonda cha mguuni huchukua Muda mrefu kupona na hatari ya kupata maambukizi ni kubwa.

Watu wenye ugonjwa wa kisukari, Matatizo ya moyo na/au ugonjwa wa figo mara nyingi mzunguko wao wa damu hupungua.

Watu wanaovuta sigara pia wanaweza kuwa na mzunguko wa damu uliopungua.

Ravi aliekatwa mguu wa kushoto anatumia Magongo aina ya Axilla kutembea.

Kutana na Ravi

Ravi ni mzee mwenye ugonjwa wa kisukari. Siku chache zilizopita; alikanyaga kipande kidogo cha kioo kilichovunjika Wakati wakati wa ndani ya nyumba yake. Kwa sababu ya hisia kidogo alizonazo katika mguu wake, hakuweza kugundua kwa Siku kadhaa. Alipogundua hilo, alijaribu kujitibu mwenyewe.

Kwa sababu ya ugonjwa wake wa kisukari, Ravi ana mzunguko mbaya wa damu kwenye sehemu ya miguu yake. Hii ilimaanisha kuwa kidonda hakikupona, na baadaye kikapata maambukizi. Maambukizi yalienea na Ravi akawa mgonjwa sana.

Familia ya Ravi ilimpeleka hospitalini ambapo aliambiwa kwamba ni muhimu kukata sehemu ya chini ya mguu wake ili kuzuia maambukizi yasienee zaidi. Ravi angeweza kufa kama asingefanyiwa hivyo.

Swali

Kuzuia vidonda vya mguuni Kunaweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kukata mguu ambao unasababishwa na vidonda vya mguuni.

Ni mambo gani ambayo yangeweza kumsaidia Ravi kuepuka kupata kidonda cha mguuni?

  • Elimu kwa Ravi kuhusu namna ya kutunza miguu yake, pamoja na kuikagua kila siku kama ina vidonda
  • Kuvaa viatu vinavyofaa ndani na nje ya nyumba ili kulinda miguu yake.

Utambuzi wa mapema wa kidonda cha mguu na matibabu yake ni njia nyingine ya kupunguza kukatwa miguu.

Ni kitu gani kinaweza kuwa kimemsaidia Ravi kuepuka kukatwa mguu?

  • Ravi angeweza kwenda kwenye kliniki yake ya afya ya mahali anapoishi mara tu alipoumia mguu wake
  • Wafanyakazi wa afya waliopata mafunzo wanaomfanyia matibabu ya mara kwa mara, na Kila baada ya Muda mfupi pamoja na wanaFuatilia kidonda chake cha mguuni.
  • Wanafanyia tathmini ya mara kwa mara ya ugonjwa wake wa kisukari pamoja na kumhudumia.

Sura isiyo ya kawaida ya mguu, kukatwa kidole cha mguuni au sehemu ya chini ya mguu

Tunaposimama, uzito wa mwili wetu hugawanywa kwa usawa kwenye miguu yetu pale inapogusa ardhi.

Wakati wa kutembea, kwa kila hatua tunayopiga, kila mguu uliokanyaga kwenye ardhi hubeba mara 1 1/2 ya jumla ya uzito wa mwili wa mtumiaji. Kugawa uzito kwa usawa ni muhimu.

Kubadilika kwa sura ya mguu Kunaweza kusababisha shinikizo kubwa sana kwenye sehemu za mguu. Hii Inaweza kusababisha kidonda cha mguuni.

Watu wenye vidole au miguu isiyo na umbo la kawaida, au watu ambao wamekatwa vidole au mguu, wako katika hatari ya kupata kidonda cha mguuni kutokana na mgandamizo kwenye kubeba uzito wa mwili wao.

Ruby amekaa kwenye kitanda cha kliniki na amenyosha miguu yake kwa Wakati wa. Mtoa huduma anachunguza miguu yake.

Kutana na Ruby

Ruby ana umri wa miaka 55 na ana ugonjwa wa kisukari. Amekatwa kidole cha mguuni kutokana na kidonda cha mguuni chenye maambukizi.

Wakati Ruby anapotembea uzito ambao hapo awali ulikuwa ukisambazwa sawa kwa mguu wake wote sasa unasambazwa kupitia sehemu ya ndogo ya mguu wake ambao ilibaki.

yuko katika hatari ya kupata kidonda kingine cha mguuni kwa sababu ya mgandamizo mkubwa kwenye sehemu iliyobaki ya mguu wake.

Ruby anahudhuria kliniki ya ugonjwa wa kisukari mara kwa mara ili kuhakikisha anadumisha afya yake na kudhibiti ugonjwa wa kisukari. Kwa kuwa yuko katika hatari ya kupata kidonda kingine cha mguuni, anahudhuria pia kliniki ya mguu wa kisukari. Ili kuzuia kuzuia kidonda kingine cha mguuni, Ruby amepewa kiatu maalum ambacho humsaidia kupunguza mgandamizo kwenye sehemu ya mguu wake iliyobaki. Hii inaitwa kiatu maalum cha kupunguza mgandamizo sehemu iliyopata kidonda. Aidha anatembea kwa kutumia magongo Yanayowekwa kwapani kusaidia kupunguza mgandamizo juu ya mguu wake.

Umekamilisha somo la kwanza!

katika Somo linalofuata utajifunza kuhusu aina tofauti za vifaa saidizi vya kusogea kutoka eneo moja kwenda eneo lingine.