Ufuatiliaji wa viti saidizi vya msalani au bafuni
Ufuatiliaji
Ni muhimu kwamba watu wajue kwamba wanaweza kuwasiliana na watoa huduma, wakapata huduma Wakati wowote ikiwa kiti saidizi chao cha msalani au bafuni kina shida.
Wateja hupata kibadiko wanapokwenda kupata baadhi ya huduma. Kibandiko hiki, kina maelezo ya mawasiliano na huduma inayohusu kifaa husika.
Kwa kawaida mtu mwenyetumia kiti saidizi cha msalani au cha bafuni; huwa ana vifaa saidizi vingine.Wakati unafuatilia kifaa saidizi chochote, angalia pia kuhusu kiti saidizi cha bafuni au msalani.
Ufuatiliaji utakusaidia kujua:
- Ikiwa kiti saidizi cha msalani au bafuni bado kinakidhi mahitaji ya mhusikamiajimiaji
- Ikiwa kiti saidizi cha msalani au bafuni kinahitaji matengenezo yoyote au kubadilishwa.
Muulize mtu Maswali yafuatayo ili kukusaidia kuelewa ikiwa kiti saidizi chake cha msalani au bafuni bado kinakidhi mahitaji yake:
- Je unatumia kiti saidizi chako cha msalani au bafuni?
- Je unapata matatizo yoyote Wakati wa kutumia kiti saidizi cha msalani au bafuni?
- Una Maswali yoyote kuhusu kiti saidizi chako cha msalani au cha bafuni?
Ikiwa mtumiaji hatumii kiti saidizi cha bafuni au msalani au ana shida kukitumia, tafuta sababu ujue ni kwa nini hawezi kukitumia. Kisha kwa pamoja tafuteni suluhisho pamoja.
Tumia maelezo ambayo umekusanya ili kuamua na mhusika kama kuna hatua zozote zinazohitajika. Hatua za kawaida zimeanishwa hapa chini.
Kukarabati au kudumisha kiti saidizi
Nati au breki zilizolegea zinaweza kukazwa kwa kutumia vifaa vya kawaida tu.
Je, unamKumbuka Daudi?
David ni mwanaume mzee na dhaifu; mwenyeishi na mke wake Leitengi.Anatumia kiti saidizi cha msalani na bafuni
Wakati wa ufuatiliaji, Daudi anaelezea kwamba kiti saidizi chake cha bafuni kinacheza wakati anapokuwa anakitumia. Unakikagua na kugudundua kuwa, mguu mmojapo kati ya miguu ambayo inaweza kuongezwa na kupunguzwa urefu, unalegea.Unaukaza na kumwongesha Daudi na mke wake Leitengi namna ya kufanya kama itatokea tena, waweze kurekebisha wenyewe. Kiti saidizi ni salama na imara sasa.
Badilisha vipuri
Ikiwa ndoo inayoweza kuondolewa ya kiti saidizi cha msalani imeharibika, inaweza kubadilishwa bila ya kununua kiti kingine
Fikiria vipuri ambavyo vinapaswa kuhifadhiwa katika ghala.
Swali
Nani anaweza kukusaidia kupata vipuri vinavyohitajika Mara kwa mara?
- Watengenezaji wanajua vipuri ambavyo vinavyohitajika wakati unapoenda kununua kifaa saidizi kipya kwa mara ya kwanza.
- Weka rekodi ya matengenezo uliyoyafanya. Kwa kufanya hivyo; utaweza kupata taarifa itakayokusaidia kuainisha aina ya vipuri vya vifaa saidizi ambavyo vinahitaji kubadilishwa Mara kwa mara
Kubadilisha kiti kisichofaa kwa matumizi
Kiti kinapaswa kubadilishwa kama kina kutu au nyufa.
Uwepo wa kutu au nyufa katika fremu au sehemu ya kukaa ya kiti waweza kuwa hatari.
Mafunzo zaidi
Mtumiaji na mtoa huduma wake wote kwa pamoja wanaweza kuhitaji mafunzo zaidi kuhusu namna ya kutumia kiti saidizi , au namna ya kukaa na kutoka juu ya kiti saidizi.
Je, unamKumbuka Aida?
Aida anatumia kiti saidizi cha msalani kinachowekwa juu ya choo Wakati wa mchana, na binti yake anamsaidia kukaa juu yake.
Wakati wa uSiku, Aida hutumia kiti saidizi cha msalani kilicho karibu na kitanda chake.
Wakati wa ufuatiliaji unamwUliza Aida 'Je, unapata changamoto yoyote Wakati wa kutumia kiti saidizi chako cha msalani au kile cha bafuni?'
Aida anaeleza kwamba wakati mwingine hawezi kwenda msalani kwa haraka ili afike kwa wakati. Hii imesababisha ahadhirike Mara kwa mara.
Unamwelezea kwamba kuanzisha utaratibu wa kwenda msalani (Wakati wa mchana\) Kila baada ya muda fulani kunaweza kumsaidia.
Aida na binti yake wanakubaliana na wewe, kwa kuanza kwenda msalani Kila baada ya masaa mawili. Aidha mnakubalina kwamba ikiwa hakutakuwa na mabadiliko, Ada anapaswa kuonana na mtaalamu wa afya ili kuhakikisha kuwa hana tatizo lingine la afya.
Kufanya tathmini kwa mara ya pili
Mtu anaweza kuhitaji kufanyiwa tathmini kwa mara nyingine; ikiwa amepata kiti saidizi cha msalani kingine, kiti saidizi cha bafuni au kama ana kifaa saidizi kingine au kama mahitaji yao yamebadilika.
rufaa
mpe rufaa kwenda kuonana na mtaalamu wa huduma ya afya:
- kama una wasiwasi kuhusu afya ya mhusikamiaji
- Mahitaji yao ya kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine; au mahitaji yao ya kwenda msalani yamebadilika sana kwa Siku za hivi karibuni.
mpe rufaa kwenda kwenye huduma nyingine ikiwa mtumiaji anaweza kufaidika na vifaa saidizi ambavyo huwezi kumpa.
mpe rufaa kwenda kwenye huduma za utengamo, ikiwa mhusika anaweza kufaidika na utengamo; Hii itawasaidia waweze kujihudumia kwenye mambo mahitaji yao binafsi.
Swali
Je unamKumbuka Cali?
Wakati wa unafanya ufanya ufuatiliaji, Cali anakuambia kuwa afya yake imedorora zaidi na anajiona kuwa hayuko salama kutumia kigoda saidizi cha bafuni. Anasimama wima kwa taabu na anapata wasiwasi kwamba anaweza kuanguka kutoka kwenye kigoda.
Je, ni hatua gani utajadili pamoja na Cali na binti yake?
- kama afya ya Cali imedhoofika zaidi, Unapaswa kumuUliza ikiwa ameonana na mtaalamu wa huduma ya afya hivi karibuni. Ikiwa sio, mpe rufaa kwenda kumuona.
- Mahitaji ya Cali yamebadilika kwa hivyo anapaswa kufanya tathmini ya kiti chake cha msalani na bafuni kwa mara nyingine
- Wakati wa kufanya tathmini, fuatilia kama kuna shughuli zingine zinampa Cali taabu katika kuzifanya. Aidha anaweza pia kufaidika na vifaa saidizi vingine.
Umekamilisha Somo la Tano!
Ikiwa una Maswali au maoni yoyote, Tafadhali yaandike kwenye jukwaa la majadiliano.