Kujitunza ni nini?
Kujitunza kunamaanisha kujihudumia mwenyewe. Moduli hii ya TAP inalenga shughuli za Kujitunza ambazo mtu hufanya kila Siku ili kuhakikisha kuwa anapata mahitaji yake binafsi ya msingi.
Baadhi ya mifano iliyozoeleka ya shughuli za utunzaji binafsi ni:
- Kuoga mwenyewe
- Kwenda msalani
- Kuvaa nguo
- Kula na kunywa
Ili kuweza kufanya shughuli nyingi zinazohusu Kujitunza mwenyewe bila kupata Msaada wa mtumiaji mwingine, watu wengi hutumia stadi za kimaumbilie kama kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kuweza kusimama bila kuyumba, nguvu na mawasiliano ya sehemu mbalimbali za mwili.
Aidha, mtu anahitaji ujuzi wa kufikiri ili kuweza kupanga na KuKumbuka kufanya kazi mbalimbali za Kujitunza.
Wakati wa kufanya kazi hizi za Kujitunza ni muhimu kuelewa ujuzi wanaohitaji kutekeleza hatua tofauti za shughuli.
Hebu tuangalie hatua na ujuzi unaohusika katika mifano miwili ya Kujitunza.
Kazi
1. Washing your body
Ni hatua gani zinazohusika katika kuoga?
Panga hatua katika utaratibu sahihi kwa kuanzia namba 1 hadi namba 6.
Hatua za kuoga mwenyewe:
- Hamia mahali ambapo utaweza kuoga mwenyewe
- Vaa
- Kusimama, kukaa au kuchuchumaa katika Wakati wakuoga Maji Yanayotoka kwenye bomba juu, kuingia kwenye Maji yaliyoko kwenye beseni, au kuegemea ndoo
- Shika sabuni na oga sehemu mbalimbali za mwili wako
- Jifute Maji
- Kuvaa nguo.
Ni stadi zipi zinatumika katika kutekeleza hatua hizi?
Stadi zote zilizotajwa hapo juu zinatumika au hatua zote zilizoko hapo juu zinafuatwa.
2. Kuvaa nguo
Hatua za kuvaa nguo:
- Kuhamia mahali penye faragha ili kuvaa nguo
- Kuchagua nguo na kuzitandaza nje
- Kuvaa nguo ikiwa ni pamoja na kufanya mambo kama vile kufunga zipu na vifungo
- Kuweka nguo ambazo ulizivaa sehemu ya mbali.
Ni stadi zipi zinatumika katika kutekeleza hatua hizi?
Stadi zote zilizotajwa hapo juu zinatumika au hatua zote zilizoko hapo juu zinafuatwa.
Kula na kunywa ni kazi nyingine za Kujitunza ambazo hutumia stadi za kimaumbile na kufikiri.
Stadi za kimwili za kuhama kutoka eneo moja kwenda eneo jingine, kusimama imara bila kuyumba na mawasiliano ya viungo vya mwili ni muhimu sana kuwa na Uwezo wa Kula na kunywa salama.
Stadi za kimwili na kufikiri huruhusu watu:
- Kupanga kile watakachokula na KuKumbuka kula Mara kwa mara
- Hamia mahali ambapo kuna watu wananakula
- Kukaa wima
- Kukatakata chakula katika vipande ambavyo vyaweza kutafunika.
- Kuweka chakula kinywani mwao (pamoja au bila kutumia vyombo)
- Kutafuna na kumeza.
Kwenda msalani kazi nyingine ya Kujitunza ambayo hutumia stadi za kimaumbile na stadi za kufikiri.
Watu wanahitaji:
- Stadi za kimaumbile kwenda kwenye choo na kukitumia
- Stadi za kufikiri kutambua na / au KuKumbuka Wakati wa kwenda msalani na kujua nini cha kufanya Wakati watakapofika huko.
Watu pia hutumia Uwezo wao wa kuzuia na kuruhusu Mkojo na haja kubwa kuepuka ajali (Kutokwa kwa haja\).
Soma juu ya kujua zaidi kuhusu kuruhusu na kuzuia Mkojo na haja kubwa.