Kusaidia watumiaji wa vifaa saidizi kuvitumia katika jamii
Kwa watu wengi, upatikanaji wa vifaa saidizi ni sehemu muhimu ya kuwa na Uwezo wa kushiriki katika shughuli ambazo wanataka au wanahitaji kufanya.
Hata hivyo, hata katika kutumia vifaa saidizi, watu wanaweza kukabiliana na vikwazo ambavyo vitaendela kupunguza Uwezo wao wa kuvitumia kikamilifu.
Vikwazo hivi vinaweza kujumuisha:
- Sehemu ambayo haifikiki kiurahisi
- Unyanyapaaji kwenye jamii na ubaguzi
- Ukosefu wa taarifa
- Ukosefu wa huduma au sera.
Kila mtu ana jukumu la kufanya kuhakikisha kwamba watu wanaotumia vifaa saidizi wanaweza kushiriki katika shughuli wanazotaka au wanazohitaji kufanya, kwa usawa kama wengine.
Kutana na Lei.
Lei alipata ugonjwa wa kiharusi na anaishi na binti yake nyumbani kwake. Upande wa kulia wa mwili wa Lei ni dhaifu, na wakati mwingine maneno ambayo anayoongea hayaeleweki kwa urahisi . Anatumia fimbo ya kuteWakati waa kumsaidia kutoka eneo moja hadi jingine.
Kabla ya kupata ugonjwa wa kiharusi , Lei alikuwa akifanya kazi katika jamii na mara nyingi aliuza mboga katika soko la eneo hilo. Hata hivyo, baada ya kiharusi chake ilikuwa ni vigumu kuingia ndani ya basi kwenda sokoni. Pia aligundua baadhi ya wanawake katika soko hilo waliacha kumshirikisha katika maongezi yao.
Lei alihisi kutengwa na alicha kwenda sokoni mara Mara kwa mara. Hata hivyo, Siku moja dereva wa basi alimwonyesha Lei kifaa saidizi cha kupanda ngazi kinachobebeka ambacho alitengeneza, na kilimsaidia kuweza kuingia na kutoka kwenye basi kwa urahisi.
Rafi yake Lei aliyeko naye pale sokoni alimsaidia kuzungumza na wanawake wengine na kuelezea kwamba Lei bado anaweza kuelewa na kushiriki katika mazungumzo. Hatahivyo, alihitaji muda zaidi wa kuzungumza vizuri zaidi. Wanawake wengine walielewa na kumjumuisha tena katika mazungumzo yao, na kuhakikisha wanampa muda wa kutosha kujibu pale alipohitaji kufanya hivyo.
Kwa mara nyingine Lei anauza mboga zake sokoni Mara kwa mara, na anafurahia kushirikiana na wanawake wengine.
Swali
1. Ni vikwazo gani ambavyo Leo Alikabiliana navyo katika usHabaririki wake kwenye jamii?
1. Lei Alikabiliana na:
- Vikwazo vya kimazingira (aligundua kuwa ni vigumu kuingia ndani ya basi)
- Vikwazo vya kimtazamo(wanawake katika soko walimbagua Lei katika mazungumzo na kazi zao).
2. Nmana gani Alivimudu? Jukumu gani watu wengine wAlifanya?
2. Alikabiliana na vikwazo wa Msaada wa watu mbalimbali katika jamii yake:
- Dereva wa basi alimsaidia Lei kushinda vikwazo vya kimazingira kwa kwa kutengeneza ngazi inayobebeka, ili aweze kuingia na kutoka kwenye basi.
- Rafiki wa Lei alimuunga mkono kuzungumza na wanawake wengine, ili wafahamu kwamba Lei bado anaweza kushiriki katika mazungumzo na shughuli zao.
Umekamilisha Somo la Nne!
Ikiwa una Maswali au maoni yoyote, Tafadhali yaandike kwenye jukwaa la majadiliano.